Huduma 01 · Website

Website Design
Website za aina tofauti, na bei zinatofautiana kulingana na aina ya website unayotaka na vitu vinavyotakiwa. Kila kitu kinajengwa kwa mkono, kinafanya kazi vizuri kwenye simu, na kinakabidhiwa kikiwa live.
Website: categories 5
Chagua kulingana na biashara yako. Kila website inafanya kazi vizuri kwenye simu, ina kitufe cha WhatsApp, na inakabidhiwa ikiwa live.
Starter
Biashara ndogo, mtu binafsi, au unayeanza mtandaoni.
- Website ya ukurasa mmoja (sehemu 5: kuhusu, huduma, picha, maoni, mawasiliano)
- Inafanya kazi vizuri kwenye simu na kompyuta
- Kitufe cha WhatsApp na fomu ya mawasiliano
- Google Maps ya eneo lako
- SEO ya msingi ili upatikane Google
- Raundi 1 ya marekebisho
Business
Kampuni yenye huduma kadhaa inayotaka kuonekana kitaalamu.
- Kurasa hadi 5 (Nyumbani, Kuhusu, Huduma, Gallery, Wasiliana)
- Design ya kipekee inayofuata brand yako
- Gallery ya picha na video
- Sehemu ya habari/blog
- Viungo vya mitandao ya kijamii + WhatsApp
- SEO ya msingi + Google Business Profile
- Raundi 2 za marekebisho
Professional
Kampuni inayopokea maombi, booking au wateja wa nje.
- Kurasa hadi 10
- Design ya kipekee kabisa, animations za kisasa
- Fomu za booking / maombi zinazotuma WhatsApp na barua pepe
- Kiswahili na Kiingereza (lugha mbili)
- Google Analytics na ripoti ya wageni
- Kasi ya juu na usalama (SSL)
- Mafunzo ya kusasisha maudhui
- Raundi 2 za marekebisho
E-Commerce
Duka la mtandaoni linalouza na kupokea malipo.
- Duka lenye bidhaa hadi 100
- Kikapu (cart) na checkout
- Malipo: M-Pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na kadi
- Taarifa ya order kwa WhatsApp na barua pepe
- Dashboard ya kusimamia bidhaa na orders
- Akaunti za wateja na ufuatiliaji wa order
- Discount codes na promotions
- Raundi 2 za marekebisho
Enterprise
Mifumo ya kipekee: portal ya wateja, booking, dashboards.
- Kurasa zisizo na kikomo
- Web app ya kipekee (portal ya wateja, mfumo wa booking, dashboards)
- Malipo ya mtandaoni + API integrations (SMS, CRM, n.k.)
- Lugha nyingi
- Watumiaji wenye majukumu tofauti (admin, staff, mteja)
- Ripoti na takwimu
- Mafunzo ya timu yako
- Msaada wa miezi 3 · Raundi 3 za marekebisho
Vitu vinavyolipwa tofauti (kwa bei ya soko): domain (.co.tz / .com), hosting ya mwaka, na ada za payment gateway. Tunakushauri na kukusimamia ununuzi wake. Matengenezo ya kila mwezi (updates, backups, mabadiliko madogo): Tsh 100,000/mwezi (hiari). Ukurasa wa ziada: Tsh 100,000.